Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi katika khutba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 29 Khordad 1405 Shamsia, iliyofanyika katika Muswala wa Quds mjini Qum, alitoa mkono wa pole kwa siku za maombolezo ya Bwana wa Mashahidi Imam Hussein (as), na kuhusu lengo la mapinduzi ya Imam Hussein (as) akasema: Imam Hussein (as) aliandika katika wasia wake kwa Muhammad ibn al-Hanafiyya:
«إنَّمَا خَرَجْتُ لِطَلَبِ الاْءصْلاَحِ فِی أُمَّه جَدِّی مُحَمَّدٍ صَلَّی اللَهُ عَلَیْهِ وَءَالِهِ؛ أُرِیدُ أَنْ ءَامُرَ بِالْمَعْرُوفِ وَأَنْهَی عَنِ الْمُنْکَرِ، وَأَسِیرَ بِسِیرَه جَدِّی وَسِیرَه أَبِی عَلِیِّ بْنِ أَبِی طَالِبٍ علیه السلام. فَمَنْ قَبِلَنِی بِقَبُولِ الْحَقِّ فَاللَهُ أَوْلَی بِالْحَقِّ، وَمَنْ رَدَّ عَلَیَّ هَذَا أَصْبِرُ حَتَّی یَقْضِیَ اللَهُ بَیْنِی وَبَیْنَ الْقَوْمِ بِالْحَقِّ؛ وَهُوَ خَیْرُ الْحَاکِمِینَ».
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Hadhrat Fatima Maasuma (as) alisisitiza kuwa; Imam Hussein (as) katika wosia huu ametaja malengo ya mapinduzi yake kuwa ni kutafuta marekebisho katika Umma wa Mtume (saww), kuamrisha mema na kukataza maovu, na kufuata mwenendo wa Mtume (saww) pamoja na Amirul-Mu’minin Ali ibn Abi Talib (as).
Khatibu wa Ijumaa wa Qum aliongeza kuwa Imam Sadiq (as) katika ziara ya Hadhrat Abbas (as) anasema:
«السَّلَامُ عَلَیک أَیهَا الْعَبْدُ الصَّالِحُ- الْمُطِیعُ لِلَّهِ وَ لِرَسُولِهِ وَ لِأَمِیرِ الْمـُؤْمِنِینَ وَ الْحـَسَنِ وَ الْحُسَینِ عليهم السَّلَامُ»
Yaani, mlolongo wa utiifu wa Hadhrat Abbas (as) unaanzia kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake (saww) na Imam Ali (as), kisha unaendelea kwa Imam Hasan (as) na Imam Hussein (as).
Alisisitiza kuwa; kutoka katika mafundisho haya mawili; yaani kuamrisha mema na kukataza maovu, pamoja na utiifu kamili kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake (saww), Maimamu (as), na katika zama za ghaiba kwa Walii Faqihi, kuna mafunzo muhimu kwa zama zetu za leo.
Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: Kwanza, mema na maovu hayajifungii katika matendo ya mtu binafsi pekee, bali yanajumuisha mifumo yote ya kisiasa, kijamii, kitamaduni na kiuchumi. Pili, kutokana na maneno ya Imam Sadiq (as), tunaelewa kwamba; moja ya sifa muhimu za mja mwema ni kwamba Muumini anapaswa kuwa mtiifu kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake (saw) na Maimamu (as).
Khatibu wa Ijumaa wa Qum aliongeza: Katika kuamrisha mema na kukataza maovu pia, yule anayeamrisha au anayekataza anapaswa kuwa mtiifu kikamilifu kwa Uislamu ili jamii isipate machafuko. Uchunguzi wa historia ya Karbala unaonyesha kwamba; Bani Hashim wote na Masahaba walikuwa watiifu kikamilifu kwa Imam Hussein (as), na katika mazingira magumu zaidi hawakusifiwa na Imam Hussein (as) kwa sababu ya ushujaa wao binafsi, bali kwa sababu ya utiifu wao kamili kwa Hoja ya Mwenyezi Mungu.
Mwakilishi wa Walii Faqihi mjini Qum aliendelea kusema: Mema na maovu ni dhana zinazobadilika kulingana na mazingira, na utambuzi sahihi wa mifano yake katika kila zama unahitaji mamlaka ya kuitambua, Katika zama za kudhihiri kwa Imam Mahdi (aj), jukumu hilo ni la Imam wa Zama, na katika zama za ghaiba ni la Walii Faqihi mwenye sifa zote zinazohitajika.
Alisema: Katika zama za ghaiba, ili kuamrisha mema na kukataza maovu kusitoke nje ya mkondo wake sahihi na kusiangukie mikononi mwa wasio na uwezo au kutekelezwa kwa misukumo ya kibinafsi, tunahitaji mwongozo wa Kiongozi wa Umma.
Imamu wa Ijumaa wa Qum alieleza kwamba; Walii Faqihi, kama Naibu wa Imam wa Zama (aj), ana jukumu la kufafanua mema na kutambua maovu ili lengo la kuleta marekebisho katika Umma wa Kiislamu litekelezwe kwa usahihi na jamii isikumbwe na mifarakano pamoja na utekelezaji wa matakwa binafsi au ya makundi.
Aliendelea kusema: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika ujumbe wake kwa wananchi wa Iran kuhusu makubaliano yaliyotiwa saini alisema: «Kimsingi nilikuwa na mtazamo mwingine, lakini kwa sababu ya ahadi ambayo Rais, akiwa Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, alitoa kwangu kwa niaba yake na wanachama wengine kuhusu kulinda haki za wananchi wa Iran na Muqawama, na kwa kuwa alisisitiza kwamba anakubali kuwajibika kwa jambo hilo, niliruhusu makubaliano hayo. Pia amesisitiza kwamba; iwapo upande wa Marekani utataka kufanya madai ya kupita kiasi, hawatakubali jambo hilo.»
Ayatullah Saidi alisisitiza: Kwa kuzingatia historia ya Marekani, tunajua kwamba haitekelezi ahadi zake. Lakini kwa kuheshimu maelekezo ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, tumedumisha mipaka inayotakiwa na tunatumaini kwamba upande wa pili utatekeleza ahadi zake, sisi, kwa kumfuata Hadhrat Abbas (as), tuko tayari kutii amri za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Hadhrat Maasuma (as) alisema: Idara ya Mahakama imechukua hatua nzuri dhidi ya majasusi, mamluki na waharibifu katika jamii, na wananchi wamefahamishwa kuhusu hatua hizo, tunatoa shukrani kwa juhudi hizo.
Ayatullah Saidi katika khutba ya kwanza alisema: Mwenyezi Mungu katika Aya ya 25 ya Suratul-Fath anasema:
«هُمُ الَّذِینَ کَفَرُوا وَصَدُّوکُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَالْهَدْیَ مَعْکُوفًا أَنْ یَبْلُغَ مَحِلَّهُ ۚ وَلَوْلَا رِجَالٌ مُؤْمِنُونَ وَنِسَاءٌ مُؤْمِنَاتٌ لَمْ تَعْلَمُوهُمْ أَنْ تَطَئُوهُمْ فَتُصِیبَکُمْ مِنْهُمْ مَعَرَّةٌ بِغَیْرِ عِلْمٍ ۖ لِیُدْخِلَ اللَّهُ فِی رَحْمَتِهِ مَنْ یَشَاءُ ۚ لَوْ تَزَیَّلُوا لَعَذَّبْنَا الَّذِینَ کَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِیمًا»
“Hao ndio walio kufuru na wakakuzuieni msiingie Msikiti Mtakatifu, na wakawazuilia dhabihu kufika mahala pao. Na lau si wanaume Waumini na wanawake Waumini msio wajua mkawasaga na mkaingia makosani kutokana nao bila ya kujua... Mwenyezi Mungu (amefanya haya) ili amuingize amtakaye katika rehema yake. Lau wangeli tengana bila ya shaka tungeli waadhibu walio kufuru kwa adhabu chungu.”
Imamu wa Ijumaa wa Qum alifafanua: Makafiri wa Makka kwa miaka mingi walikuwa wakiwazuia Waislamu kuingia Makka, katika tukio la Hudaibiyya, Waislamu walipokuwa wakielekea Makka kwa ajili ya Hijja, makafiri waliwazuia kuingia ili kutekeleza ibada hizo, kutokana na hilo, Waislamu waliamua kukabiliana na Makuraishi kwa nguvu zote, lakini Mwenyezi Mungu kupitia Sulhu ya Hudaibiyya alizuia umwagaji damu huo na hakuwaruhusu Waislamu kuishambulia Makka.
Alisema: Ndani ya Makka kulikuwa na wanaume na wanawake waliokuwa wameingia Uislamu lakini walificha dini yao kwa makafiri wa Makka na hawakuwa na uwezo wa kuhama kwenda Madina. Ikiwa Waislamu wangeishambulia Makka, Waislamu hao wangeathirika, ndio maana Mwenyezi Mungu aliwazuia Waislamu kupitia Sulhu ya Hudaibiyya na kuwajumuisha Waislamu wa Makka katika rehema Yake.
Khatibu wa Ijumaa wa Qum aliongeza: Sulhu ya Hudaibiyya pia ilileta manufaa na ushindi mwingine mwingi, ndio maana Mwenyezi Mungu ameiita katika Suratul-Fath kuwa ni “Ushindi Ulio Wazi”.
Alisema kwamba; Suratul-Fath inasimulia tukio la kihistoria, lakini pia ina mafunzo mengi katika zama zetu za leo, kisha akayafafanua mafunzo hayo.
Funzo la Kwanza: Umuhimu wa Kulinda Maisha ya Waislamu
Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: Kulinda damu za Waislamu ni muhimu zaidi kuliko kushambulia na kupigana na makafiri. Kwa maneno mengine, kulinda maisha ya Muumini hata kama kutasababisha kucheleweshwa kwa ushindi mkubwa wa kijeshi kwa Waislamu, bado kulinda maisha hayo kunapewa kipaumbele, hili linaonesha kwamba; Uislamu ni dini ya upendo na urafiki, si dini ya kutafuta nguvu.
Funzo la Pili: Kupima Vipengele Vyote Kabla ya Mgongano
Mwakilishi wa Walii Faqihi mjini Qum alisema: Uongozi unapaswa kuhesabu kwa makini pande zote, athari na matokeo ya mapambano dhidi ya adui, kisha utoe amri ya kushambulia, ikiwa vita vingetokea huko Hudaibiyya, mbali na madhara ambayo yangewapata Waislamu, manufaa mengi pia yangepotea.
Funzo la Tatu: Umuhimu wa Vita vya Masimulizi
Khatibu wa Ijumaa wa Qum aliongeza: Katika vita vya simulizi na taarifa, Waislamu hawapaswi kuruhusu maadui kuwa wa kwanza kuwasilisha simulizi yao, ndio maana Mtume Mtukufu (saww) kupitia Sulhu ya Hudaibiyya aliwanyima maadui nafasi ya kutumia vibaya tukio hilo na akauthibitishia umma kwamba; Waislamu si watu wa kupenda vita, ingawa wanajua namna ya kupigana.
Funzo la Nne: Kuonesha Uzuri wa Uislamu Ulimwenguni
Alisema: Uongozi wa hekima wa Mtume (saww) ulionesha ni wakati gani upanga unapaswa kutolewa na ni wakati gani vita vinapaswa kusitishwa, ili Uislamu uonekane kwa sura nzuri zaidi mbele ya watu ulimwenguni.
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Hadhrat Maasuma (as) alisema: Leo pia, usimamizi wa hekima wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi umetufikisha kwenye ushindi mbele ya ubeberu wa kimataifa, na sisi tunaendelea kuwa watiifu kwa uongozi huo huku tukisubiri ushindi wa mwisho.
Maoni yako